Teuvo Kopra:

 

 

Pepo wa
udhaifu

 

 

”Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa.” (Lk 13:11)

 

Huyu mama alikuwa ameinama, haku­weza kunyosha mgongo.

Tulisoma kwamba alikuwa na roho ya udhaifu, yaani pepo ya udhaifu.

Hii ni roho ya aina gani?

 

 

Yesu alimponya mwanamke

 

 

Yesu alipokuwa duniani miaka elfu mbili iliyopita, aliponya wagonjwa wengi mbalimbali.

Mambo hayo yalikuwa na maana kubwa kwa mgonjwa, kwani alipata afya.

Pia ilionyesha wale walioona uponyaji huo au kusikia ukuu wa Yesu.

Kwa sababu ndani ya Biblia imeandikwa juu ya uponyaji mbali mbali zina ujumbe muhimu kwetu tunaposoma Biblia.

 

Siku ya sabato alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo. Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa. Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako.  Akaweka mikono yake juu yake, naye akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu. Basi mkuu wa sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akajibu, aka­waambia mkutano, Kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe katika siku hizo, wala si katika siku ya sabato. Lakini Bwana akajibu akasema, Enyi wanafiki, kila mmoja wenu, je! hamfungui ng´ombe wake au punda wake siku ya sa­bato katika zizi, aende naye kumnywesha? Na huyu mwa­namke, aliye wa uzao wa Ibrahimu, ambaye Shetani amemfu­nga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwa kifungo hiki siku ya sabato? Aliposema haya wakatahayari wote walioshindana naye; mkutano wote wakafurahi kwa sababu ya mambo matukufu yaliyotendwa na yeye. (Lk 13:10-17)

 

Huyu mama alikuwa ameinama, haku­weza kunyosha mgongo.

Tulisoma kwamba alikuwa na roho ya udhaifu, yaani pepo ya udhaifu.

Hii ni roho ya aina gani?

Siyo roho ya pepo tu kwani Yesu angeli­kemea.

Huyu mama hakuugua mgongo tu kwani Yesu angemponya.

 

Yeye alikuwa na matatizo ya kiroho.

Matatizo yake ya ndani yalikuwa na nguvu hadi yakamdhuru mwili wake baadaye.

Labda kwanza alikuwa na matatizo makali.

Labda baadaye alipata pia majaribu ma­kubwa.

Hata akawa na majuto makubwa.

 

Labda aliyumba kimawazo akapata hali ngumu.

Alipokuwa na matatizo hayo yote alianza kupinda.

Alianza kutembea ameinama baadaye aliinama kabisa.

Baadaye mwili wake ulizoea hali ya ku­pinda.

Yeye mwenyewe hakuweza kujinyosha ka­bisa.

Hali yake ikawa ya huruma na yakusiki­tisha sana.

 

Siku hizi watu wengi wana hali hiyo rohoni au ndani yao.

Kwa hali ya nje tunawaona wakiwa na hali nzuri na afya njema.

Wanaonekana kwamba mambo yao yote ni mazuri.

Lakini utu wa ndani ya watu wengi ina hali ya kupinda.

Utu wa ndani wa mtu ina hali kama ya huyu mama wa Biblia, aliyepinda wala asiyeweza kujinyosha mwenyewe.

 

Hakuna anayetaka kuwa kilema wa jinsi hii, lakini huyu mtu hawezi kujipa msaada.

Mtu wa kiroho wa watu wachache wana­enenda kwa kuinama wakiwa wamei­namisha vichwa vyao. 

Angetaka awe mkristo mwenye nguvu anayeendelea mbele kwa njia ya ushindi na kumbe yeye ni kilema kiroho.

Ana udhaifu wa kiroho.

 

Sasa nataka kutoa maswali manne.

Swali la kwanza: Mtu anaingiaje katika udhaifu wa kiroho?

Swali la pili: Mtu mdhaifu kiroho anaishi maisha gani?

Swali la tatu: Tunaondokanaje na udhaifu wa kiroho?

Na swali la nne: Tunatunzaje uhuru tu­liopata?

 

Sitoi maswali tu, bali tunatafuta majibu ya maswali haya manne.

Tunatafuta majibu ili tuweze kujihadhari ili tusiingie katika udhaifu wa kiroho.

Na tukiingia humu, tutatokaje?

 

Tumesoma Luka sura ya kumi na tatu na sasa tunatafuta majibu kutoka katika sura hii.

Swali la kwanza lilikuwa: Mtu anaingiaje katika udhaifu wa roho?

 

Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dha­bihu zao. Akawajibu akawaambia, Je! mwadhani ya kwamba Wagalilaya hao walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote, hata wakapatwa na mambo hayo? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo. Au wale kumi na wanane, walioangukiwa na mnara huko Siloamu, ukawaua, mwadhani ya kwamba wao walikuwa wakosaji kuliko watu wote waliokaa Yerusalemu? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo. (Lk 13:1-5)

 

Tulisoma kuhusu Wagalilaya waliotoa dhabihu kwa Mungu.

Ndiyo maana walitoa dhabihu ya kondoo au dhabihu nyingine kwa ajili ya dhambi zao.

Ndipo Pilato aliwaua na kuchanganya damu yao na damu ya ile dhabihu.

Hayo yalikuwa mambo mabaya sana yali­yoongelewa na watu wengi.

Wengine walisema: "Hao Wagalilaya walikuwa ni wenye dhambi sana ndiyo maana ilikuwa lazima kwao kuteseka hivyo."

Watu walifikiri mtu akiteseka sana ni kwa sababu yeye ni mwenye dhambi sana.

Yesu alisema kwamba hawakuteseka kwa sababu ya hiyo.

Watu walielewa mambo vibaya.

Walikuwa na elimu potofu juu ya dhambi na matokeo ya dhambi.

 

Tulisoma pia katika mstari wa nne, kwamba siku moja ajali kubwa ilitokea karibu na birika ya Siloamu.

Siloamu inapatikana Yerusalemu upande wa kusini wa Hekalu.

Pale Siloamu kulikuwa na mnara ulio­anguka juu ya watu na watu kumi na nane walifariki katika ajali hiyo.

Hapo tena watu waliwaza kwamba hawa watu waliopata ajali walikuwa na ma­kosa kuzidi wengine.

Watu walifikiri: Ndiyo maana waliteseka.

Yesu alisema walikuwa hawana makosa zaidi ya wengine.

Tena Yesu alionyesha kwamba watu ha­wakuelewa katika mafundisho ya dhambi.

Watu walifikiri kwamba matatizo na ajali kubwa zinatokana na dhambi.

 

Pia sikuhizi watu wanafikiri: Ukipata matatizo au ajali kubwa ni kwa ajili ya dhambi.

 

Wanafunzi wa Yesu walikuwa na mafu­ndisho mabaya ya aina hiyo pia.

 

Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi ali­yetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwa ki­pofu? Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake. (Jh 9:1-3)

 

Wanafunzi walifikiri huyu mtu alizaliwa kipofu kwa sababu mtu amefanya dhambi.

Tena Yesu alikataa mafundisho yao yenye makosa.

Watu walifikiri kwamba kama kuna ma­tatizo, magonjwa au ajali, hayo ya­natoka na dhambi mwanadamu alizo­fanya.

Matokeo ya dhambi ni matatizo, walifikiri.

 

Biblia inasema wafuasi wa Yesu wana matatizo mengi.

Hatusomi, lakini Paulo alisema katika Wa­raka wa Rumi, kwamba tufurahi katika dhiki pia; tukijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; (RUM 5:3)

Na pia Biblia inasema katika Matendo ya Mitume:

... na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi. (MDO 14:22)

 

Watu wachache wanafikiri kinyume kwamba mtu akiendelea vizuri hiyo ni ishara kwamba mambo yake ni mazuri mbele za Mungu na si lazima atubu.

 

Mafundisho hayo sio sahihi kuhusu dhambi na matokeo yake.

Watu wanaelewa Biblia vibaya.

Pia wanamwelewa Mungu vibaya.

Wengi wanaelewa upatanisho wa Yesu vibaya.

Tungeadhibiwa kwa ajili ya dhambi zetu sisi sote tungalikufa.

Sisi sote tumefanya dhambi.

Biblia inasema Yesu aliadhibiwa kwa ajili ya dhambi zetu.

Sisi hatuadhibiwi kwa ajili ya dhambi zetu, kwani tayari Yesu ameadhibiwa.

Mtu akiwa na matatizo na majaribu Mungu ameyaruhusu lakini hayo siyo adhabu juu ya dhambi zetu au unyonge wa imani yetu.

 

Watu wote wana matatizo na majaribu.

Matatizo na vikwazo vingine siyo ishara ya kwamba sisi wenye dhambi zaidi ya watu wengine.

Watu wote wana matatizo.

Pia ambao wameokoka na wasiookoka.

Tukiwa na maisha mazuri siyo ishara kwamba mambo yetu yote ni sawa na Mungu na kwamba si lazima sisi ku­tubu.

Mambo ya nje hayatujulishi kuhusu dhambi zetu au kwamba tumeishi vizuri.

Tukiwa na mafundisho yasiosahihi katika mambo haya, yanatupeleka katika unyonge wa roho.

 

Njia nyingine ambazo zinasababisha unyonge wa roho inapatikana katika Luka, sura ya kumi na tatu, mstari wa sita hadi wa tisa.

 

Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate. Akamwambia mtunzaji wa shamba la mi­zabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiha­ribu? Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi; nao ukizaa matunda baa­daye, vema! la, usipozaa, ndipo uukate. (Lk 13:6-9)

 

Tulipookoka tulipandwa katika shamba la mizabibu ya Mungu.

Baadaye Mungu anasubiri tukue kiroho.

Tusipokua Mungu anaanza kulima maisha yetu.

Maana yake ni nini?

Udongo wa mioyo yetu inageuzwa na yanatafutwa magugu.

Mungu anaupalilia.

Yaani Roho wa Mungu anaanza kutafuta mambo yaliyofichwa, dhambi zilizo­fichwa.

Dhambi zinazuia kukua kwetu kiroho.

Sawa na mambo mengine.

 

Tusiposoma Biblia au kuomba hatuwezi kukua kiroho vizuri.

Tukiacha wakristo na kanisa, hatukui kiroho vizuri.

Mungu anapolima maisha ya ndani yetu, analainisha ugumu wetu.

Mara nyingine anaweka mbolea, yaani sa­madi.

Ni mfano kwamba anatoa baraka kubwa.

Mungu anafanya haya yote ili tukue ki­roho na tutoe matunda ya kiroho.

Tunda la roho na kukua kiroho ina maana gani?

Ni mabadiliko ya maisha.

Mazoea ya dhambi yanabaki kwa aliye­okoka.

Labda mtu kabla ya wokovu alisema uongo, aliiba na aliwadanganya watu na kufanya mabaya mengi.

Baada ya kuokoka Mungu anataka kwamba maisha ya mtu yanabadilika.

Dhambi zinasahaulika na tabia za rohoni zinaanza kuonekana.

Hivyo ni kukua kiroho.

Mungu anataka hayo kutoka kwetu.

Haya yasipofanyika Mungu anaanza kutu­jenga mwenyewe maisha yetu.

 

Tukiwa na mafundisho sahihi juu ya dhambi na upatanisho na adhabu ya dhambi na jinsi ya kukua kiroho ha­tuingii katika udhaifu wa kiroho.

Hii ni jibu la swali la kwanza, kwamba mtu anaingiaje katika udhaifu wa kiroho?

Mafundisho mabaya juu ya dhambi na upatanisho na kutokuwa kiroho, ya­namwelekeza mtu kwenye udhaifu wa kiroho.

 

Swali la pili lilikuwa mtu mnyonge wa kiroho anaishi maisha ya aina gani?

 

Yeye hapati ushindi wa kiroho.

Yeye hapati nyingi jibu katika maombi yake.

Mungu hawezi kuongea na mtu anayeishi maisha ya udhaifu kiroho.

Ujumbe wa Biblia haifunguki kwake.

Yeye hana shukrani wala roho ya imani.

Maono yake sio ya mbinguni bali ya du­niani katika mazingira magumu.

Mdhaifu kiroho hakui kiroho.

 

Swali la tatu lilikuwa tunaondokanaje na udhaifu wa kiroho?

Tulisoma Biblia jinsi gani Yesu alimponya aliyekuwa na roho ya udhaifu.

Sasa tuone mwanamke alivyofunguka na tunatafuta mfano kwa maisha yetu na tunaondokanaje na udhaifu wa kiroho.

 

Tumesoma sura ya kumi na tatu ya Injili ya Luka.

Mstari wa kumi na moja unasema kwamba mwanamke alikuja kwenye mkutano wa Yesu.

Alijua Yesu tu anaweza kumsaidia.

Alikuwa ametafuta msaada mahali pengine lakini hajapata.

Yesu akamwambia: Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako.

Mama alipomsikiliza Yesu alipata imani.

Hivyo ni muhimu tuongee na kuhubiri ili wasikilizaji waweze kutuelewa na kuamini kwamba Yesu ana nguvu za kuponya na kusaidia.

Imani ya mwanamke iliongezeka Yesu alipoweka mkono juu ya kichwa chake.

Mara akainuka akamshukuru Mungu.

Mwanamke alipata msaada baada ya kuja kumsikiliza Yesu alisikiliza na kua­mini.

Akaja mbele akapona na kumshukuru Mungu.

 

Hapa kuna fundisho kwetu.

Yesu anaweza kutusaidia.

Ni vyema tumtafute tukiwa na udhaifu wa kiroho.

Tunapowaona ndugu na dada wenye ma­tatizo tusiwahukumu bali tujaribu kuwapeleka kwa Yesu.

Tuwalete mikutanoni ibadani tuwa­ombee nao kuwaongoza kwa Yesu.

 

Mama alipopata msaada kutoka kwa Yesu alimshukuru Mungu.

Hata na wengine wengi walimshukuru.

Furaha yao ilikuwa ya pamoja.

 

Tulisoma katika mstari wa kumi na nne hadi mstari wa kumi na saba kwamba siyo wote waliofurahi.

Msimamizi wa sinagogi alifikiri kwamba sasa Yesu amefanya vingine tunavyo­fanya katika sinagogi yetu.

Yesu alivunja tabia walizokuwa nazo.

Yesu hakushika sabato alivyotaka mwa­ngalizi wa sinagogi.

 

Mtu fulani anapookoka au mtu anapo­umbwa upya watu wengi wanafurahi.

Lakini wengine wanaweza kusema huyu amekuwa mwenye dhambi sana, huyu hawezi kuwa mmoja wetu.

Au ikiwa mkristo ameanguka na anahitaji utakaso watu wanaweza kumwadhibu kwa makosa yake.

 

Ni vizuri tukumbuke kwamba Yesu ali­adhibiwa kwa ajili ya dhambi zetu.

Mtu anapookoka au anatakasika wengi wanafurahi lakini sio wote.

Watu wachache hawatamkubali.

Jamii wanaweza kumkataa au watu wengine.

 

Huyu mama alipopata msaada hakurudi nyuma.

Ingawa mwangalizi wa sinagogi alijaribu kumpinga mama hakuomba unyonge imeru­die.

Mama hakumwombea Yesu ampe unyonge wake tena ile mwangalizi wa sinagogi aweze kumkubali na ili kupingwa imalizeke.

 

Hata wewe usikubali kukataliwa kwa ajili ya imani yako.

Ukiwa umewekwa huru kwa imani ile ambayo Yesu mwenyewe amefanya usiache uhuru wako.

 

Pia tulisoma kwamba Yesu alimkaripia mwangalizi wa sinagogi na wengine waliopinga uponyaji.

Ni vizuri tukumbuke kwamba hata kama tunakataliwa na wengine Yesu yuko upande wetu.

Bwana asifiwe!

 

Swali la nne ni tunatunzaje uhuru huo?

 

Tunaelewa kwamba tunaweza kuutunza kwa kujihadhari na mambo yale yana­yosababisha udhaifu wa kiroho.

Tukisikiliza mafundisho ya Yesu hatuta­kuwa wanyonge kiroho.

Na tukipata mafundisho mazuri juu ya dhambi na utapatanisho na matokeo ya dhambi.

Na pia tunda la roho likiwa ndani yetu.

Hivyo hatutakuwa udhaifu kiroho.

 

Biblia inaendelea kufafanua juu ya jambo hili.

 

Kisha alisema, Ufalme wa Mungu umefanana na nini? nami niufananishe na nini? Umefanana na punje ya haradali aliyotwaa mtu akaitupa katika shamba lake; ikamea, ikawa mti; ndege wa angani wakakaa katika matawi yake. (Lk 13:18,19)

 

Mtu anapookoka anakuwa raia wa ufalme wa mbinguni.

Sasa Yesu anazungumzia mfano wa kwamba imani ni kama punje ya hara­dali.

Mbegu ndogo inayotoa mti mkubwa.

Hivyo hata imani iliyohai inaota.

Isipoota ina matatizo.

 

Naye alikuwa akipita katika miji na vijiji, akifundisha, katika safari yake kwenda Yerusalemu. Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia, Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze. (Lk 13:22-24)

 

Mtu fulani alimwuliza Yesu wanaookoka kuna wengi au wachache tu?

Yesu hakutoa jibu bali alisema: Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba

Alitaka kusema kuokoka hakutoshi bali waliookoka wakaze mwendo kwa imani.

Sisi tukue kiroho.

Haitoshi kuokoka tu bali uendelee hadi mwisho katika imani.

 

Halafu mistari minne inayofuatia Yesu anaeleza juu ya wale waliokuwa wame­okoka, lakini baadaye wakaacha imani na Yesu kabisa.

 

Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;  ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu. Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu. Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi we­nyewe mmetupwa nje. (Lk 13:25-28)

 

Hapa Yesu haisemi juu ya wakristo wa­nyonge wala walioanguka bali juu ya wale walioacha imani yao.

Wamemwacha Yesu na hawataki tena kuendelea na njia ya imani.

Wakifa bila imani hawana maisha ya mi­lele.

Bali wao ni wale waliookoka lakini ha­wakuendelea hadi mwisho katika njia ya wokovu.

 

Halafu Yesu anaongea juu ya mambo ya­jayo na matokeo hukumu ya mwisho.

 

Nao watakuja watu toka mashariki na magharibi, na toka kaskazini na kusini, nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu.  Na tazama, wako walio wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, na wa kwanza watakaokuwa wa mwisho. (Lk 13:29,30)

 

Hapa tunaelezwa juu ya ufalme wa Mungu, inayotajwa sana ndani ya Biblia.

Tunasafiri kuelekea ufalme huo.

Sisi tuliookoka na tunataka tuendelee hadi mwisho katika imani.

Sehemu ya waliookoka ni safi.

 

Siku hizi watu wengi wana matatizo ya udhaifu wa kiroho.

Na watu wachache wameacha imani yao siku hizi.

Yesu anaonya kwamba mtu ye yote hata­baki kwa hali ya unyonge na baadaye akaanguka kabisa.

Mtu wa jinsi hiyo mwisho wake unakuwa ni mbaya.

Pia Luka sura ya kumi na tatu inatuku­mbusha kwamba Yesu anataka kutu­saidia na kutuweka huru na udhaifu wetu.

Na anataka kutulinda tusiingie humu, bali tungesafiri kwa nguvu mpaka Mbinguni.

 

 

Mungu akubarikie!

 

 

-----------------------------------------------------------------