Ujumbe wa Ufunuo – sura ya 2.
Ujumbe kwa Efeso
Ujumbe kwa Smirna
Ujumbe kwa Pergamo
Ujumbe kwa Thiatira
Katika sura mbili zifuatazo kuna ujumbe kwa makanisa saba. Ujumbe huo inatuhusu sisi pia. Tungeweza kuchunguza kila kanisa na ujumbe wake na kutafuta mafundisho kwa ajili ya wakati wetu na makanisa yetu. Tungepata mafundisho mazuri na maonyo makali. Kukaripia na shukrani.
Lakini uchunguzi huo ungechukua muda mrefu, hata sasa hatutachunguza ujumbe kwa makanisa saba kwa upande huo bali tunachunguza kwa upande wa unabii yaani kwa mpangilio wa muda. Kwa njia nyingine kila kanisa inawakilisha muda wake kikristo tangu wakati wa mitume hadi mwisho wa kipindi cha makanisa. Wakati wa Yohana ujumbe kwa makanisa ulikuwa ni unabii wa mambo yajayo, kwamba wokovu na ukristo na kukua vitakuwaje. Sasa tunaweza kuangalia nyuma, lakini kipindi hicho waliangalia mbele. Sasa tunaweza kwanza kusoma unabii ndani ya Ufunuo na kisha tuangalie katika historia ya makanisa kama mambo hayo ni kweli kadri ya Ufunuo wa Yohana. Tukichunguza mambo kwa njia hii tutagundua ni kweli kwa kadri ya Ufunuo.
EFESO (miaka 30-100)
Wakati wa makanisa kanisa la Efeso lilikuwa kanisa la kwanza. Kanisa la Efeso ni mfano nzuri wa makanisa wakati wa mitume. Yale mambo yaliyokuwa Efeso yalipatikana hata katika makanisa mengine ya wakati huo. Matatizo ya Efeso yalikuwapo hata sehemu zingine na shukrani zilizopatikana Efeso zilikuwa faida kwa makanisa mengine. Efeso inawakilisha wakati wa mitume, tangu mwaka wa thelathini hadi mwaka wa mia moja baada ya Kristo.
1. Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. 2. Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; 3. tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka. 4. Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza. 5. Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu. 6. Lakini unalo neno hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia. 7. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu. (UFU 2:1-7)
Makanisa ya wakati huo yalikuwa pungufu na kupungukiwa, kama siku hizi pia. Tulisoma mstari wa kwanza kwamba Yesu alitembelea kati ya vinara, yaani katikati ya makanisa. Alipenda kukaa ndani ya makanisa yale yote saba katika Ufunuo. Kwa sababu Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele (EBR 13:8) hata leo anatembelea makanisani. Ni vizuri tukikaa ndani ya makanisa yetu sababu Yesu anatembelea makanisani.
Wakati wa mitume makanisa yalikuwa na matukio mengi kazi nyingi na uvumilivu. Wakati huo uliangaliwa sana kwamba dhambi isikubaliwe maishani. Wale mitume wa uongo walijaribu kujiingiza miongoni mwao. Lakini waliteswa na waliojifanya walitengwa kando. Wakristo waliudhiwa sana kwa ajili ya Jina la Yesu lakini hawakuchoka. Baadaye upendo wao kwa Yesu ulipoa na uamusho ukaanza kupoa. Miujiza haikutokea kama hapo awali. Labda haikutafutwa tena. Pole pole hata kazi ya Roho Mtakatifu makanisani ilipungua na kazi za watu ziliongezeka.
Yesu aliahidi kutoa kinara mahali pake iwapo upendo hautarejea ndani ya wachungaji na wahubiri. Hema ya kukutania ni mfano mkubwa katika Agano la Kale. Katika hema ya kukutania kilikuwamo kinara pia. Kazi ya kinara na zile taa ilikuwa kumulika ile meza ya mikate iliyokuwa kule mbele. Mifano hiyo inamaana ya vyakula vya rohoni ambavyo Mungu anataka kutugawia makanisani. Mungu anataka kwamba katika makanisa kuwe na chakula cha rohoni lakini kama upendo wa waalimu umepoa kwa Yesu, waalimu na wahubiri hawaioni tena ile meza ya chakula, na hawawezi kuwagawia wakristo chakula cha rohoni. Hapo waalimu na wachungaji na wakristo watapata njaa ya kiroho. Hayo yote yanasababishwa na upendo wa Yesu kupoa ndani ya wachungaji.
Historia ya makanisa inatuelewesha kwamba pole pole makanisa yalianza kujitoa, hawakutunza ile nguvu waliyokuwa nayo. Yaani hawakutubu.
Hivyo uamsho ulianza kupungua moto katika karne zilizopita na makanisa mengi yalianza kwenda pembeni na uongozi wa Roho Mtakatifu. Kinara kilitolewa mahali pake, chakula cha kiroho kilipungua makanisani. Kama chemchemi ya rohoni ilienda pembeni na kukauka, Mungu alifungua zingine na uamsho wa kiroho mpya. Kila mara kuna makanisa yenye nguvu na yale yaliyokauka.
Wachunguzi wa Biblia wanafikiri kwamba shemasi mmoja wa Yerusalemu kwa jina Nikolao (MDO 6:5) baadaye alianguka na kuleta mafundisho ya uzushi. Lakini hatujui, wala si muhimu kujua. Pia watu walifundishwa kwamba kazi za utumishi walipewa baadhi ya watu. Wakristo wa kawaida walikatazwa kufanya kazi ya Mungu na kushuhudia. Mafundisho hayo yalileta maisha ya ukahaba na uhuru wa mwili. Waliambiwa kwamba tumewekwa huru kutoka utumwa wa dhambi, tunaishi tunavyotaka, dhambi haitatuangamiza. Walisema: Upatanisho unatosha. Hivyo mwili ulipewa uhuru wa kuishi unavyotaka katika uchafu.
Ni kawaida kwamba wengi walipoteza imani yao kwa sababu ya mafundisho ya aina hiyo.
Mawazo ya aina hii na uhuru wa mwili ulichukiwa mwanzoni huko Efeso, na hata Yesu alichukia, kama tulivyosoma. Yesu alikataa ukuhani tofauti bali wote ni watendakazi wake siyo makuhani peke yake. Hivyo kila mmoja ana wajibu wa kutangaza Injili na siyo watumishi tu. Baada ya mafundisho ya Wanikolai kuenea, walitokea mababa wa kanisa na majengo ya Wakatoliki.
Kutokea kwa kanisa la Katoliki kulisababisha kanisa la Efeso kwenda pembeni. Yesu anaelekeza somo hili kwa mtu mmoja mmoja akisema, kwamba: Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. (UFU 2:7a) Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu. (UFU 2:7b)
Ushindi haupatikani bila mapambano. Yeye atakayepambana na kushinda, kuna ahadi nzuri kwa ajili yake. Yeye asiangalie wakristo wengine bali apambane mbele za Mungu wake. Hata wengine wakianguka, wewe usianguke. Usiwaige wengine kama siyo wazuri.
Efeso inatupa mfano wa wakati wa kiroho, ambayo ilikuwa wakati wa Yohana. Mwaka wa thelathini hadi mia moja baada ya Kristo.
SMIRNA (miaka 100-313)
Baada ya kanisa la Efeso barua ilikuja kwa kanisa la Smirna. Kanisa la Smirna linawakilisha wakati na maisha ya kiroho kuanzia mwaka wa mia moja baada ya Kristo na kuendelea kama miaka mia mbili mbele, kutukaribia sisi. Kwa usahihi hadi mwaka wa mia tatu kumi na tatu baada ya Kristo.
Smirna ni sawa na Mirha, yaani manemane. Manemane ni mfano wa mateso. Kanisa la Smirna ni la wakati wa mateso, ilipata dhiki nyingi kwa ajili ya imani yake.
8. Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai. 9. Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani. 10. Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima. 11. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili. (UFU 2:8-11)
Karne ya kwanza sehemu nyingi Wayahudi na Wanasariti, yaani wafuasi wa Yesu, walikutanika ndani ya sinagogi moja. Mara nyingine Wayahudi waliwapinga wafuasi wa Yesu na mara zingine waliwakubali. Baadaye Wayahudi sehemu zote walianza kuwapinga na kuwachukia wafuasi wa Yesu. Hata makaisari wa Rumi waliwapinga na kuwatesa.
Tulisoma, kwamba kanisa liliambiwa kwamba nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. (UFU 2:10b) Tungeweza kusoma katika historia kwamba kuanzia mwaka wa sitini na tatu hadi mwaka wa mia tatu kumi na mbili tunaona kwamba muda wa dhiki uligawanywa vipindi kumi yaani "siku kumi"!
Kanisa halikukemewa tu bali watu walitiwa moyo pia. Matezo yalimalizika baada ya kaisari Konstantino kukiri dini ya kikristo kuwa dini ya kiserikali. Mateso yaliisha na wakati huo wakristo walifikiri kwamba utawala wa Mungu wa miaka elfu moja umefika, sababu hawateswi tena. La hasha, wakati wake ulikuwa bado.
Smirna inawaelezea wafia Kristo waliopeleka kanisa mbele. Kanisa linawakilisha muda baada ya Efeso yaani mwaka wa mia moja hadi mwaka wa mia tatu kumi na tatu baada ya Kristo.
PERGAMO (miaka 313-500)
12. Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo Anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili. 13. Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani. 14. Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini. 15. Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile. 16. Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu. 17. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea. (UFU 2:12-17)
Huko tunapata kanisa jingine linalofuata mwaka wa mia tatu kumi na tatu hadi mia tano baada ya Kristo. Kanisa la tatu ni Pergamo. Maana ya jina la Pergamo ni: Maisha ya ndoa. Siyo ndoa halali yaani aina ile tunaoelezwa kwenye Biblia, bali isiyo halali. Yaani kuishi kama ndoa halali, lakini kihalali siyo ndoa. Ndoa ambayo hajafungwa kihalali. Biblia inaita maisha haya ni uasherati. Huo siyo mpango wa Mungu, kama ndoa.
Wakati wa Pergamo ulikuja baada ya wakati wa Smirna. Wakati wa Pergamo uliendelea kama miaka mia mbili hivi mpaka mwaka wa mia tano.
Mateso yaliisha baada ya dini ya kikristo kuanzishwa kama dini ya kiserikali. Katika mataifa mengi serikali inatetea dini fulani na wakuu wa serikali wanaamua mambo ya makanisa pia. Wale viongozi si lazima wawe na wokovu. Wanaweza kuwa wenye dhihaka.
Mateso yaliisha na Wakristo wa Pergamo walifurahi na kusema: "Sasa utawala wa Mungu wa miaka elfu umeanza. Furaha yao haikudumu muda mrefu kwani kilicho gunduliwa kilikuwa "ndoa isiyohalali". Historia inaeleza wapagani walianza kuingia makanisani. Wao walikuwa wengi na kwa sababu mambo yalifanyika kwa kupiga kura, wao waliokuwa wengi walishinda.
Pole pole wale wasiookoka walianza kuwatesa wale wakristo waliokuwa kanisani.
Katika mstari wa kumi na tatu unatuambia kwamba ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani. Wapergamo wasiookoka waliabudu sana miungu mingine. Madhabahu ya sanamu Zeu ya ilikuwapo huko na hekalu la Asklepios. Zeu alikuwa sanamu aliyeabudiwa kama mungu wa mbingu na mwanga. Pia alikuwa mungu wa sanamu kwa wale wote. Watu waliamini hivi. Asklepios alikuwa akasimamia matibabu. Ishara yake ilikuwa nyoka aliye hai.
Mji huu mdogo uliongozwa kwa ibada za sanamu yenye nguvu. Kwa sababu watu waliobudu sana sanamu hiyo ilimaanisha adha na mateso kwa wakristo. Walio wa Yesu walipata shida, lakini hawakumkana.
Tulisoma kuhusu mtu moja Antipa. Historia ya kikatoliki inatueleza kwamba Antipa alibatizwa akiwa na miaka kumi na tatu, alikufa akitetea wokovu akiwa na miaka tisini na tisa.
Mafundisho ya Balaamu yaliingia kanisani. (Mstari 14) Yaani mtu anaweza kuwa wa dini fulani, ingawa hana toba ya kweli. Hii siyo sahihi, hii ilikuwa uhuru wa mwili. Kanisa lilikubali uasherati na mialiko yake. Pia mafundisho ya Wanikolai yalikubaliwa, hayo yalichukiwa huko Efeso. Watu waliishi kwa njia ya ukahaba na walitegemea kwamba neema yatosha. Yesu alichukia na kukataa mambo haya. Hata wachungaji walikuja juu ya wakristo. Zamani wachungaji waliwahudumia wakristo lakini sasa walitawala.
Tusome Petro wa kwanza sura ya tano, mistari ya pili na tatu.
2. lichugeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. 3. Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi.
Siyo kama wajifanyao mabwana,... bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi. Hata sisi tunasumbuliwa na mafundisho ya Wanikolai. Sisi tena siyo watumishi wa kanisa na wakristo bali tunataka kuwatawala. Wachungaji wanahudumia kanisa kwa kuwagawia mazuri, maarifa ya rohoni na chakula cha rohoni. Mafundisho ya Wanikolai yalileta utawala mbaya kanisani ambayo Yesu aliyachukia na anachukia siku hizi pia. Wapergamo walikemewa kwa kukubali mambo hayo.
Kanisa lilikuwa hivyo wakati wa Pergamo. Yaani wakati wa mia tatu hadi mia tano. Kanisa Katoliki lilianza hivi taratibu.
THIATIRA (miaka 500-1500)
Kanisa la nne ni la Thiatira. Hii ilikuwa baada ya wakati wa Pergamo. Muda wa Thiatira ulichukuwa miaka elfu moja. Muda wa Thiatira ulichukua wakati wa kanisa la katoliki. Kuanzia mwaka wa mia tano mpaka wakati wa Lutheri kama miaka elfu na mia tano.
18. Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana. 19. Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza. 20. Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. 21. Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake. 22. Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake; 23. nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake. 24. Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, wasiozijua fumbo za Shetani. kama vile wasemavyo, sitaweka juu yenu mzigo mwingine. 25. Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja. 26. Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamalaka juu ya mataifa, 27. naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu. 28. Nami nitampa ile nyota ya asubuhi. 29. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. (UFU 2:18-29)
Baadhi ya wakristo wa Thiatira walipata sifa na wengine walikemewa. Historia inaeleza kwamba uamusho ulitokea sehemu mbali mbali na makanisa mengine yalizaliwa. Makanisa ya macahche yalipotea zaidi na mafundisho ya Biblia na hata Roho Mtakatifu. Makanisa hayo yalikufa kiroho. Ndiyo maana baada hayo baadhi walipata shukrani na wengine kukemewa. Uamsho ulileta watu kwa Yesu na uliongoza watu kwenda mbinguni na uamsho ulishukuriwa. Yale makanisa yaliyokufa yaliyopotosha watu upotevuni yalikemewa.
Thiatira alikuwa na mpotoshaji, jina lake ni Yezebeli. Yeye alikuwa mwanamke aliyejiita nabii. Wengi walimfuata yeye na waliangamia pia. Yezebeli ni mfano wa dini ya kikatoliki aliyeleta kule kanisani kuabudu Maria. Kanisa Katoliki linawafundisha watu kwa mafundisho ya Maria.
Thiatira walikuwepo wakristo wengi wale waliopewa ahadi nzuri za ushindi. Ukatoliki ulikuwa mkubwa na ulikuwa ni kanisa lililopotoka. Watu wengi walipotea pia. Lakini watu wachache hawakupotea. Tena Mungu alikuwa pamoja na wale waliotaka kumfuata. Historia inaeleza kwamba uamusho ulitokea sehemu mbali mbali.
Mambo ya kanisa la Thiatira yalikuwa na unabii wa kuzaliwa kwa katoliki. Ufunuo huo ulikuwa kamili.
Turudie kwa ufupi.
Kanisa la Efeso linawakilisha historia ya wakati wa mitume yaani mpaka mwaka wa mia moja baada ya Kristo. Smirna tokea mwaka mia moja hadi mia tatu kumi na tatu. La tatu ni Pergamo, inawakilisha miaka ya mia tatu kumi na tatu hadi mia tano. Ya nne ni Thiatira. Matukio yake yalibashiri dunia ya ukiristo itakuaje miaka ya mia tano hadi elfu moja mia tano. Sasa tunaona kwamba Ufunuo ulitimia kimaandiko.
---------------------------------------------------------------------------------------------------------