Teuvo Kopra:
Ujumbe wa Ufunuo
Kwanza
Neno la Mungu lina utajiri mwingi.
Neno moja linaweza kuangaliwa kwa njia nyingi tofauti na tunapata mawazo mapya kwa neno hilo. Hii inatueleza ukuu wa Mungu na utajiri unaomo ndani ya Biblia. Akili za Mungu hatuzitambui ila kwa sehemu ndogo. Ni hivyo hata katika Kitabu cha Ufunuo.
Kimefafanuliwa kwa njia tofauti. Pia inategemea hali yenyewe. Pia kuna tafsiri mbali mbali ambazo mtu mwenyewe ametafsiri kadri ya kuelewa kwake. Hizo hazijapewa msisimuko na Roho Mtakatifu lakini tunaweza kuzigundua na kuzielewa.
Tusingekuwa na Kitabu cha Ufunuo hatungeelewa yanayoendelea sasa. Hatungejua ubaya ulioko duniani. Hatungeelewa ni kwa nini Mungu anakubali yale yanayotendeka duniani. Bila ya Kitabu cha Ufunuo hatungejua mwisho wa dhambi na shetani ingekuwa kwa utinyo sana kuelewe. Lakini katika Ufunuo tunaambiwa kwamba kila kitu kibaya kina mwisho wake. Bila ya Kitabu cha Ufunuo hatungeelewa kuhusu vita, uhalifu na mateso makali ya nayowapata wanadamu.
Tukisoma Biblia tangu mwanzo mpaka mwisho tutaona kwamba Ufunuo ni kilele cha mambo yote ya Biblia. Tunaona katika Ufunuo kwamba shabaha ya Mungu ni nini. Kitabu hiki kinawafariji wanaoudhiwa na kuteswa na wanaoona mateso ya aina mbali mbali kwa kumfuata Yesu. Pia katikati ya masumbufu ya kila siku, kitabu hiki kinatupa matumaini ya mambo yajayo kwamba siku moja huzuni yote itakwisha.
Tukiangalia huku na huku na kuona uovu ulivyozidi, mateso na kumdhihaki Mungu, tunajua kwamba mambo yatabadilika upesi. Wanaodhihaki watapata hukumu yao na ubaya pia sehemu yake. Wafuasi wa Yesu watapata thawabu na mazuri yajayo.
Wengine wanataka kupinga Kitabu hiki cha Ufunuo. Wao wanasema hayo ni mambo tu siyo kweli, hayatafanyika. Ni mifano tu.
Lakini tukisoma Biblia nzima tunaona kwamba, tabia ya Mungu iko kama mifano iliyotofautishwa na yale yaliyotendeka na sisi hatuwezi kuyachanganya. Pia hata yale ya kweli yana maana yake na hapo tunaona utajiri wa Biblia. Mambo mengine madogo katika Ufunuo yameshatimia, hata kwa kujirudia. Huo ni utangulizi. Matukio kamili na ya mwisho yatakuja baadaye, wakati ukifika. Sura zile za kwanza za Ufunuo zimekwisha timia.
Sasa hivi tunaishi wakati wa unabii wa Mungu katika sura ile ya tatu.Wakati ule Yohana alipopata Ufunuo katika kisiwa cha Patmo huo wote ulikuwa unabii. Baadhi ya mambo mengine yamekwisha timia. Yohana alitabiri nasi tutaangalia jinsi ufunuo huo ulivyolenga sawa.
Ufunuo 1.
Ufunuo aliyopewa Yohana
Salamu kwa makanisa saba
Njozi ya Mwana wa Mtu
Sura ya kwanza ni utambulisho wa Ufunuo mzima ufafanuzi na maelezo. Sura hii ni sura ya utangulizi, au dibaji. Tukisoma na kuamini yale yaliyoandikwa katika sura hii hivyo yalivyoandikwa tunaendelea kuchunguza mambo mengine katika Ufunuo.
Hapo ndipo tutakapopata ujumbe ule ambao Roho Mtakatifu anataka kutupa. Lakini tukianza kuitafsiri kwa njia tofauti tangu mwanzo tukifikia mwisho tutakuwa mbali na ukweli na kupotea kabisa.
1. Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana; 2. aliyelishuhudia Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani, mambo yote aliyoyaona. (UFU 1:1,2)
Mungu alimpa Yesu Kitabu cha Ufunuo, malaika alikabidhi kwa Yohana naye akatuandikia sisi.
Kwa nini?
"awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi" (mst 1)
Yeye anawaonyesha watumishi wake - siyo ulimwengu. Ndiyo maana wasioamini hawawezi kukielewa Kitabu cha Ufunuo.
Tulisoma: "kwamba hayana budi kuwako upesi" (mst 1)
Wakati wa kupatikana kwa kitabu hiki mambo yalikuwa yameshaanza. Wakati wa makanisa ulikuwa tayari. Lakini baada ya wakati wa makanisa matukio mengine yatafanyika upesi na kwa muda mfupi sana.
3. Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu. (UFU 1:3)
Tunaposoma Kitabu hiki uheri wetu unaongezeka ingawa hatuelewi kila kitu.Uheri unaongezeka zaidi kadiri ya kuelewa kwetu ujumbe huo. Pia kama ujumbe huo utapata nafasi ndani ya maisha yetu uheri unazidi zaidi. Ndiyo maana tungependa kusikia ujumbe huo mioyoni mwetu na siyo tu kwa masikio.
4. Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi; 5. tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake, 6. na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina. (UFU 1:4-6)
Mistari hii ni kwa makanisa saba. Yohana alichapisha barua saba za Ufunuo kwa kila kanisa barua moja. Lakini kwa sababu Ufunuo uko katika Biblia mambo hayo yanatuhusu sisi pia, na siyo makanisa saba ya Asia tu.
Tulisoma kwamba Yesu kutuosha dhambi zetu katika damu yake. (mst 5) Ili tuelewe kitabu hiki lazima tuelewa kuhusu upatanisho ambao umefanyika kwa sababu ya upendo kwa ajili ya wenye dhambi na pia wanaoishi katikati ya hukumu ya Ufunuo.
Yesu ni "mkuu wa wafalme wa dunia." Mwingine anasema kwamba wala haifanani hivyo. Lakini Yesu ndiye mwamuzi na anayeweka mipaka kwa waovu hata wanashindwa kuivuka. Ni lazima dunia ijiandae kwa hukumu, ndiyo maana hata wabaya wanaachiwa uhuru wa kuyafanya mambo yao. Lakini ni kwa muda uliyowekwa tu.
4. Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya. (MIT 16:4)
Matukio katika Kitabu cha Ufunuo hayawezi kutokea iwapo ubaya haupo. Wapagani wanahitajika ili malengo na hukumu ya Mungu viweze kutimia. Ubaya utakapoenea zaidi au unatosha, Mungu ataumaliza. Tulisoma: ... na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu. (mst 6) Bado hatuna ufalme unaoonekana, lakini tunaambiwa katika Ufunuo utakavyokuja na utachukua muda gani.
Pia Ufunuo inatueleza ni nani watakaotawala huko na utachukua muda gani na utageukaje kuwa ufalme wa milele, yaani Mbingu mpya.
7. Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina. (UFU 1:7)
Hapa tunaelezwa kurudi kwa Yesu. Sisi pia tunaongelea mara kwa mara jambo hili. Hapa hatuelezwi kurudi kwa Yesu tunakokusubiri sasa, ila ni yale tuliyoandikiwa katika Ufunuo sura ya kumi na tisa. Kuja kwa Yesu tunakokusubiri kutafanyika kabla ya kurudi kwake, kama tulivyosoma ni wakati ambapo wote watamwona na wakati huo pia ataanzisha utawala wake wa miaka elfu moja ya amani hapa duniani.
Yesu atarudi, kama tunavyokusubiri kurudi kwake kutatokea ghafla na hivyo hawataona kwa macho. Juu ya kurudi kwa Yesu tunakokusubiri sasa, tusome sehemu mbili katika Biblia.
16. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 17. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. (UFU 1:16,17)
Yaani kwanza Yesu atarudi na waliookoka waliokufa watafufuliwa. Yaani miili yao iliyozikwa itafufuka. Halafu wale waliohai yaani wakristo watanyakuliwa kwenda kumlaki Bwana mawinguni. Baada ya hapo tutakaa naye milele. Kwanza kwenye harusi Mbinguni baadaye hapa duniani katika utawala wa Mungu wa miaka elfu moja.
Baadaye milele Mbinguni.
51. Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, 52. kwa dakika moja kufumba na kufubua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. (1KOR 15:51,52)
Wale wakristo waliokoka hapa wakati wa kurudi Yesu hawataonja mauti bali watabadilika. Mabadiliko haya ni makubwa na yako sawa au yanakaribiana na kifo na ufufuo. Haya yatatokea ghafla kufumba na kufumbua. Hapa tunaambiwa kuhusu unyakuo, ambao utatokea kwa ghafla na kwa siri sana. Wakati ule yeye hatafunuliwa kwa ulimwengu. Lakini Ufunuo sura ya kwanza mstari wa saba inatuambia kwamba kurudi kwake dunia nzima watamwona. Yeye hatakuja kunyakua bali kuanzisha utawala wa amani hapa duniani. Ataandamana na bibi arusi ambaye atakuwa amekwisha nyakuliwa.
8. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliekuwako na atakayekuja, Mwenyezi. (UFU 1:8)
Msemo "Alfa na Omega" kwa Kiebrania una maana ya herufi ya kwanza na ya mwisho katika alfabeti. Sisi tungeweza kusema "A na Z". Mwanzo na mwisho na herufi zingine hapa katikati. Mungu ni wa zamani, sasa na wakati ujao.
9. Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu. (UFU 1:9)
Wakati Kitabu cha Ufunuo kilipoandikwa kaisari Domitiani alikuwa akitawala. Wakati huo dunia nzima ilikuwa chini ya utawala wa Rumi. Kaisari Domitiani alitawala mwaka wa themanini na moja mpaka tisini na sita baada ya Kristo. Alikuwa anapinga imani ya Kikristo na pia alikuwa mtesaji. Ndiyo maana alitoa amri Yohana apelekwe kisiwa kilichoitwa Patmo. Sikuhizi kinaitwa Patino. Baada ya kaisari Domitiani kaisari Nerva alitawala dunia nzima.
Alitawala Rumi mwaka wa tisini na sita mpaka tisini na nane baada ya Kristo. Yeye alikubali Injili na hata akamtoa Yohana kule kisiwani.
Tunaona kwamba Mungu alimweka mamlakani kaisari aliyempinga Yohana na kumweka kisiwani ili aweze kupokea ujumbe wa Ufunuo huko. Kwa hivyo kaisari Domitiani alihusika ili Yohana apate Ujumbe. Baada ya Ujumbe kupatikana kaisari alitolewa mamlakani na Mungu alihitaji kaisari mwingine aliyemleta Yohana pamoja na ule ujumbe wa Ufunuo kwa watu. Hapa tunagundua kwamba ni Mungu anayeamua kuhusu utawala wo wote ule wa wafalme hata serikalini. Wao wanaabudu mipango mikubwa ya Mungu. Yeye anamwinua fulani kutawala na kumwondoa mwingine.
Patmo yaani Patino ni kisiwa kidogo kama kilomita arobaini za mraba. Huko Yohana alikuwa peke yake na aliweza kupewa ujumbe huo wa Ufunuo.
10. Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu, (UFU 1:10)
Ninafikiri kwamba hapa "siku ya Bwana" ni Jumapili. Tangu wakati wa mitume Jumapili ilisherehekewa kama siku ya kufufuka kwa Yesu. (MDO 20:7) Yaani siku ya Bwana Yesu Kristo alipofufuka kutoka wafu baada ya kusulubiwa. Katika sehemu zingine siku ya Bwana maana yake ni siku ile ya ghadhabu. (2THE 2:2, YOE 2:1-11, ISA 13:9-13, AMO 5:18-20, SEF 1:14-18)
Yohana alipokuwa kisiwani siku ya Jumapili alisikia sauti kubwa ambayo bila shaka aliifahamu.
11. ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba Efeso, na Smirna, na Pergamo na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia. 12. Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu; 13. na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa mshipi wa dhahabu matitini. 14. Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto; 15. na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi. 16. Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking´aa kwa nguvu zake. (UFU 1:11-16)
Kumbe Yohana alisikia sauti kama ya baragumu. Aliona katika maono vinara saba vya dhababu. Na katikati ya vile vinara aliona mtu mfano wa Mwanadamu, yaani Yesu na nyota saba hayo yote yalikuwa katika mkono wa kulia wa Yesu. Hata ingawa Yohana alikuwa amemwona Yesu hapo awali, ameegemea kifuani mwake wakati wa chakula cha mwisho na pia alimwona baada ya kufufuka kwake, maono hayo yalikuwa na nguvu sana alishindwa kustahimili. Hapo awali Yesu alikuja hapa duniani na Yohana alikuwa mmoja wa wanafunzi wake, Yesu hapa duniani alikuwa kama mtumwa, akawa kama mwanadamu. Lakini sasa alichukuwa mwili wake wa utukufu ndiyo maana Yohana alishindwa kumwangalia. Na sasa Yohana anatueleza hali aliyokuwa nayo baada ya kuona yale maono.
17. Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, 18. na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. (UFU 1:17,18)
Yesu alisema: "Usiogope!" Hatuna haja ya kuogopa mambo haya kwenye Ufunuo hasa waliookoka. Kama mahubiri yetu yatawafanya watu waogope inamaana kwamba hatujafaulu katika kutafsiri na kuchunguza Ufunuo. Tumekosea.
Sasa tusome sehemu muhimu sana mstari wa kumi na tisa.
19. Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo. (UFU 1:19)
Mstari huu tunaweza kuutumia kama ufunguo katika kutafsiri Ufunuo. Kama tutatumia mstari huu kutafsiri Kitabu kizima tutapata tafsiri iliyosahihi.
Mstari huo una sehemu tatu:
Kwanza: Uandike uliyoyaona, yaani Yohana alimwona Yesu, vinara vya taa saba na zile nyota saba.
Pili: Uandike .. nayo yaliyopo. Yaani ni wakati gani unaendelea sasa, wakati Yohana alipokuwa Patmo. Ulikuwa wakati wa makanisa. Wakati wa makanisa ulianza tangu siku ile ya Pentekoste na kuendelea wakati wa matukio huko katika kisiwa cha Patmo kama miaka sitini. Siku hizi wakati wa makanisa bado unaendelea. Ufunuo sura za pili na tatu zinatueleza juu ya wakati wa makanisa.
Na mambo ya tatu yalikuwa: Uandike.. yale yatakayokuwa baada ya hayo. Yaani ni nini kitakachotokea baada ya hapo kitugani kitatokea baada ya wakati huo wa makanisa, mambo hayo Yohana aliandika katika sura ya nne mpaka sura ya ishirini na mbili.
20. Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba. (UFU 1:20)
Zile nyota saba ni wahubiri, wazee wa makanisa na viongozi wengine makanisani. Vile vinara saba vina maana ya makanisa ya palepale. Kinara kimoja ni kanisa moja. Biblia inatueleza katika Agano la Kale zaidi kuhusu kinara. Hapo kuna taa saba zinazowekwa mahali pake. Mtu anapookoka taa yake inawashwa. Mafuta ni uhai wa Mungu, taa ni mioyo yetu. Yesu alizumgumzia kiango na taa katika Injili ya Mathayo.
15. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. (MT 5:15)
Tuliposoma, kwamba kiango ni mfano wa kanisa la pale pale, tunagundua kwamba Yesu alitaka kusema kwamba mtu anapookoka mahali pake ni kwenye kiango yaani kanisani.
Endelea sura ya 2.
Ujumbe kwa Efeso
Ujumbe kwa Smirna
Ujumbe kwa Pergamo
Ujumbe kwa Thiatira
-------------------------------------------------------------------------
(Hubiri 801)